Hii
imetokea Florida Marekani ambapo mtu mmoja alikua anaruka akiwa na
Parachuti lakini akakutana na ndege hii ndogo ambayo baada ya kumgonga
walianguka chini wote huku ndege ikiangukia pua.Pamoja
na ajali hii, hakuna mtu aliepoteza maisha ila wote walipata majeraha
madogomadogo baada ya kuanguka kwenye umbali wa futi 75 na wakapelekwa
hospitali ambapo mwenye Parachuti John Frost (49) aliruhusiwa kuondoka.Hili
tukio limenaswa jinsi lilivyotokea kwa sababu kulikua na mpiga picha
aliekua na camera karibu na alikua anashuhudia kila kitu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook
Post a Comment