BAADA ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya kutaka kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na kumjibu kuwa na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema katika mila za Kiafrika, posa haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.
“Nimesikia habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu yeye kama yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na masharti huzingatiwa, afuate utaratibu tu,” alisema Wolper.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment