Mahakama
imetoa hukumu kwa Nahodha na jumla ya wenzake kumi na nne kwa
kupatikana na hatia ya uzembe uliopelekea meli kuzama na kuua watu 300.
Nahodha Lee Joon-seok amehukumiwa
kifungo cha miaka 36 kwa kosa hilo, Park ambaye alikuwa injinia wa meli
hiyo amehukumiwa miaka 30, na wenzao kumi na watatu wamehukumiwa miaka
20 kila mmoja kwa kosa la uzembe uliopelekea vifo vya watu hao.
Ajali hiyo ilitokea Aprili 16 mwaka huu
Korea Kusini, ambapo meli hiyo Mv Sewol ilipata ajali ikiwa na abiria
zaidi ya 470, ambapo kati yao zaidi ya watu 300 walifariki wengi wao
wakiwa ni wanafunzi.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment