Mshambuliaji kutoka nchini Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana jioni alikabidhiwa tuzo ya ufungaji bora katika bara la Ulaya baada ya kuibuka kinara wa upachikaji wa mabao kwenye ligi ya nchini Hispania msimu uliopita.
Ronaldo alifunga mabao 31, katika ligi ya nchini Hispania, baada ya kumuacha mbali mpinzani wake Lionel Messi ambaye alikabiliwa na majeruhi na mara kwa mara.
Hata hivyo tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyokabidhiwa Cristiano Ronaldo amechangia na mshambulaiji mpya wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez ambaye kwa msimu uliopita aliifungia Liverpool mabao 31 katika ligi ya nchini Uingereza.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment