Mapenzi hatare sana!hayana cha wewe mzuri,au una cheo,au unapesa,ama
hauna...yaani yakikukamata utajuta so mtu akifikiaga maamuzi ya hivi
usimcheke kabisa!!....sawa na kumtukana mamba huku mto bado hujavuka
Huyu ni mwanafunzi aliefahamika kwa jina moja la Moza alie mwaka wa
kwanza katika chuo cha Uhasibu TIA Mkoani Singida amenusurika kufa baada
ya jaribio la kutaka kujiua kwa kujichoma na kisu kushindikana,tukio
hilo limetokea jana baada mwanafunzi huyo kumfumania mpenzi wake wa
kiume akiwa na mwanamke mwingine.....sasa ni hivi huyu mwanafunzi
akitoka hospt unaweza kumshauri vipi ili asirudie kufanya kitendo
hicho??maana huwezi kujua labda bado anayo dhamira ya
kujimalizia......ila wanaume mnapata dhambi sana kwa Mungu dah!hivi
mwanaume akiwa na mwanamke mmoja itakuwaje??au ataonekana
mshamba??....yaani tangu jana niliwaza hili tukio mpk basi...dwah
ngachoka mie!
Post a Comment