Siku chache baada ya mazishi ya kipa na nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa kuzikwa baada ya kuuwawa na majambazi mchezaji mwingine wa timu ya taifa ya Afrika kusini amevamiwa na majmbazi nyumbani kwake .
Majambazi watatu ambao bado hawajafahamika walivamia nyumba anakoishi kiungo mshambuliaji wa Bafana Bafana Sibusiso Vilakazi ambako walipora vitu kadhaa vya thamani .
Kwa mujibu wa ripoti iliyothibitishwa na mchezaji mwenyewe , majambazi hao walivamia nyumba ambamo mchezaji huyo anaishi na wanae na walimuulizia mchezaji huyo kana kwamba wanataka kumdhuru.
Hata hivyo wazazi wawili wa Sibusiso waligoma kutaja mahali ambako mchezaji huyo alikuweko hali iliyowafanya majambazi hao kuondoka bila kumdhuru mtu yoyote .
Wakati mkasa huu ukitokea Vilakazi alikuwa amelala usingizi kwenye nyumba iliyoko hatua chache toka iliko nyumba iliyovamiwa na hakutambua chochote kilichokuwa kinaendelea hadi aliposimuliwa asubuhi yake .
Vilakazi ambaye ni nahodha wa klabu ya Bidvest Wits ameelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo hasa ukizingatia kuwa bado hajasahau kilichomkuta mchezaji ambaye alikuwa akilala naye kwenye chumba kimoja kwenye kambi ya timu ya taifa Senzo Meyiwa .
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment