IMG_7411.JPG
Mama Ashura akishusha kichapo hicho. Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, timbwili hilo ‘hevi’ lilijiri kwenye banda la chipsi la jamaa aliyetajwa kwa jina la Jerome Bertin Mushi almaarufu Babu lililopo jirani na Soko la Mji Mpya mjini hapa ambapo mwanamke huyo alifanikiwa kuondoka na beseni la kuku na chipsi.
ZAMANI kulikuwa na kasumba kwamba wanaume ndiyo huwapiga wanawake lakini hivi karibuni kibao kimegeuka ambapo mama mjasiriamali, aliyetajwa kwa jina moja la Mama Ashura ambaye ni mfanyabiashara wa viazi mviringo, anadaiwa kuwapa kipondo njemba watano kisa deni.
Baada ya zogo kuwa kubwa huku umati ukifurika eneo hilo, mmoja wa mashuhuda hao alimtonya mwanahabari wetu ambaye alifika fasta na kushuhudia mama huyo akipambana vilivyo na kundi la wanaume hao ambao aliwashinda nguvu kwa kuwashushia ngumi za kutosha.

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top