WATU kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea usiku huu katika maeneo ya Gereji, External - Ubungo jijini Dar es Salaam kati ya lori na daladala aina ya DCM.
Abiria wa daladala waliojeruhiwa ni wengi mno japo idadi kamili bado haijafahamika huku juhudi za uokoaji zikiendelea kwenye eneo hilo la ajali.
Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni daladala kujaribu kuhama upande wake na kuingia upande wa pili ambapo lilikutana na lori lililokuwa kwenye mwendo mkali na kuligonga kisha kupinduka.
DCM hilo liliamua kuhama upande baada ya kukuta mbele yake limepaki daladala lingine lililokuwa limegongana na gari dogo aina ya Toyota Harrier.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment