Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amechafuka baada ya mtu anayejitambulisha kwa jina lake, kujinadi kwa kujitongozesha katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
 Amanda huyo feki amekuwa akijiuza bila aibu katika mtandao huo kwa kujitongozesha kwa wanaume, kitu kinachomuumiza muigizaji huyo ambaye pia anawashangaza wasanii wenzake juu ya tabia hiyo ya kuchefua.

“Yaani nimekuwa nikiulizwa sana, lakini juzi ndipo nilishtuliwa na msanii mwenzangu, nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba kuna mtu ananichafua kupitia mtandao, mashabiki wangu watambue kuwa mimi sijawahi kujiuza na ninajiheshimu,” alisema Amanda.

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top