Mshambuliaji Mbwana Samatta.
HUU utakuwa ni mwaka wa neema kwa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya zimeonyesha nia ya kumchukua. 

Habari za uhakika zimelifikia gazeti hili kuwa, timu nne kati ya hizo ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na Italia, zimeonyesha nia ya kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania. 
“Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa na mawasiliano kupitia meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP Mazembe,” kilieleza chanzo kutoka Ufaransa.“Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa, lakini tunaamini Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.” 
Baada ya taarifa hizo, gazeti hili lilifanya juhudi za kumpata meneja wake, Jamal Kisongo ambaye alitoa ushirikiano.“Kweli kuna timu zinamhitaji, kama nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa kwenda kufanya majaribio, badala yake kujiunga na timu na kuanza kazi. 

“Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa na mawasiliano na uongozi wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,” alisema Kisongo akionyesha kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo.
Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe. 

Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alikuwa akifanya juhudi kuhakikisha Samatta anabaki Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo amehakikisha anakwenda mbele zaidi ili kupata mafanikio zaidi.

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top