Mzazi ukiridhika na mienendo ya mwanao mbele ya macho ya watu, basi ujue ndivyo upendavyo na ni staili ya maisha uliyomchagulia mwanao kuishi leo na kesho. Mtoto huyu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5hadi 6, akifanya yasiyotarajiwa na wengi waliokuwa wakimshuhudia kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni, wakati akijinyonganyonga mauno kuendana na miondoko ya bendi ya Twanga Pepeta wakati ikitoa burudani.
Kulingana na umri wa mtoto huyu wengi hawakutarajia kuona yale aliyokuwa akiyafanya na kuwashangaza wengi huku mama yake (kulia anayeonekana nusu) akifurahia na kumpigia makofi kumshangilia. Je kwa starehe hizi na 'mafyongo haya' mtoto huyu atasoma kweli???? na je mzazi ukimkuta nafanya yasiyostahili ukiwa wewe haupo utamuadhibu ama utamchekea..
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment