Siku za mwizi ni arobaini na ikifika arobaini za mwizi anaweza kujikuta kwenye kitanzi kwa njia ambayo hata mwenyewe haamini… Hii story inatokea Newport, South Wales, jamaa mmoja amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuingia kwenye nyumba moja kwa lengo la kufanya uhalifu japo hakufanikiwa kukamilisha lengo lililomuingiza kwenye nyumba hiyo.




Matthew Waters alikutwa kwenye chumba cha spare akiwa amelala kwenye kitanda kilichopo kwenye chumba hicho huku pembeni yake kukiwa na kopo tupu la Ice Cream ambayo inaonekana aliilamba kabla ya kupitiwa na usingizi.



Matthew aliamka kwa mshtuko baada ya mwenye nyumba hiyo Julie James aliporudi kutoka kazini na kufungua mlango wa chumba hicho ambacho ana kawaida kukikagua kila mara akirudi toka kazini.


Matthew Waters

Baada ya kushtuka, Matthew alikimbia lakini alikamatwa baada ya sura yake kuonekana kwenye camera za CCTV, Mahakama ilimkuta na hatia baada ya mpelelezi wa makosa ya jinai kugundua kuwa amekuwa akiishi kwa kuvamia nyumba za watu na kuhukumiwa kifungo cha miezi nane jela na kumlipa Julie paundi 100 (sawa na Tshs 270,000/-)

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top