Ishu
ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile
anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini
kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.
Sasa hii ya leo inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni hamsini duniani Gurmeet Ram Rahim Singh
anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za
kuwashawishi wafuasi wake 400 kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa
karibu na Mungu.
Wafuasi wa Singh
walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye anaimiliki
ambapo kwenye headlines nyingine mhubiri huyu amekuwa akihusishwa na
mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na kutuhumiwa kwa
unyanyasaji wa kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa.
Mmoja wa wafuasi wake, Hans Raj Chauhan
aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za siri kwa sababu
alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza utaratibu
huo uioanzishwa Singh.
Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wanaotekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu.
ANGALIA HAPA JINSI WASANII WANAVYOJIUNGA NA FREEMASON
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment