Katika kusheherekea sikuuu ya mwanamke Duniani, Mwanamuziki mwenye hadhi ya kipekee bongo, Judith wambura mbibo maarufu kama Lady jaydee ame share story yake fupi kuhusu bifu lililowahi kutokea miaka ya nyuma kati yake na Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha.
Akitiririka kwenye ukurusa wake wa Instagram, staa huyo ambaye hana mpinzani ndani ya Bongo Fleva, alikiri kutofautiana na mwanamama huyo, baada ya madam ritha kumpaka make up lady Jaydee ambapo Jide alikuwa akiifuta hali iliyompelekea Madam kumgombeza hali iliyozua tafrani kwa mwanamuziki huyo, na kusababisha ugomvi ambapo bifu hilo lilidumu kwa mda Wa miaka mitano bila mastaa hao kuongeleshana wala kusalimiana.
Hata hivyo staa huyo amekiri kumaliza tofauti yake na mwanamama huyo kwa kudai ulikuwa ni utoto na sasa hivi bifu kati yao limeisha.
Source: Lady Jaydee
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment