Kuna namna mbalimbali ya kusupport harakati, unaweza ukabeba bango lako mwenyewe, au siku hizi teknolojia, unaweza ukaingia zako tu Twitter halafu unaweka hashtag, basi unakuwa umetoa support yako ya nguvu.
Hawa jamaa wa Uturuki wameona isiwe tabu, wameingia zao na wenyewe mtaani wakiwa wamevaa zao sketi za wanawake ili tu ku show support yao ya nguvu kwa wanawake ambao walikuwa wakiandamana kulaani mauaji ya mwanamke mmoja Ozgecan Aslan ambaye aliuawa na mwanaume aliyetaka kumbaka.
Wanawake wakaingia mtaani kudai haki zao kwa kuwa kitendo hicho kilionyesha ukatili na unyanyasaji wa wanawake kwa hali ya juu, wanaume wanaosupport nao wakaongeza nguvu kwa kuvaa sketi pia na kuandamana.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment