Baba mtarajiwa amezungumza kwa mara ya
kwanza juu ya kuishi bila kuwa na uso na kwa namna gani anahofia juu ya
hali atakayozaliwa mtoto wake mtarajiwa.
Anaitwa Mohammad Latif Khatana, 32,
kutoka Kashmir, India, hawezi kuona wala kufanya kazi kutokana na ngozi
zilizofunika uso wake. Watu humkimbia barabarani kutokana na hali yake
huku wakionekana kuogopeshwa nayo.
Kwa sasa ni mwenye faraja kutokana na
ukweli kwamba mke wake ni mjamzito wa miezi saba, ila ana hofu labda
huenda mtoto wake anaweza kuzailiwa akiwa anfanana naye.
Alisema: “Naingoja kwa
hamu hii hali ya kuwa baba na kupata furaha ya maisha. Ila nahofu kila
siku na kusali ili mwanangu asije kuzaliwa kama mimi.”
Latif, ambaye anaishi
milimani na mke wake mwenye miaka 25 aitwaye Salima, eneo la Tuli Bana,
ndani ya Jammu and Kashmir, huwa anatembea mpaka Srinagar mara nne kwa
mwaka kwa ajili ya kuomba misaada na ili kupata hela.
Alizaliwa na kinundu
kidogo kwenye uso wake ila kimeendelea kukua na ktengeneza tabaka kubwa
la ngozi kwenye paji la uso wake, linalomfanya ashindwe kuona.
Anasema: “Mama yangu bado analia kila
aniangaliapo, anajiona kama mtu mwenye kosa na anashindwa kuelewa kwa
nini mtoto wake wa mwisho amekuwa hivi.”
Latif ni mdogo kati ya wakaka wawili na dada watatu huku yeye pekee akiwa na tatizo hilo.
Bila ndugu zake angeweza kuishi maisha ya upweke sana udogoni kutokana na kutokuwa na marafiki.
“Hakuna aliyetaka
kucheza na mimi utotoni,” akaongeza. “Wavulana kijijini kwangu walikuwa
wananipiga na kunitesa kila siku. Nilipoteza jicho langu la kushoto
nilipokuwa na miaka minane na wakawa wananiita mjinga mwenye jicho
moja.”
Alipokuwa kijana Latif
alikumbana na changamoto mbalimbali za kimaisha. Ni mtu mwenye nguvu
zake ila kutokana na kushindwa kuwa anaona na kwa namna uso wake ulivyo
hakuna aliyeweza kumpa kazi.
Alisema: “Ningependa
kufanya kazi ya uhakika kama wanaume wengine wanavyofanya ili kuweza
kuzitunza familia zao, ingenifanya nijisikie fahari sana, ila hakuna
aliyenipa nafasi. Inabidi niombe na naamini watu wanaweza nisaidia ili
niweze kulisha familia yangu.”
Miaka minne iliyopita Latif alikutana
na mwanamke wa maisha yake, awali wazazi wake walijitahidi sana
kumtafutia mke ila hakuna msichana liyejitokeza, mpaka Latif aliposikia
kuhusu Salima.
“Mke wangu ana mguu mmoja tu na kwa
muda mrefu amekuwa akitafuta mume, punde tulipokutana tulijua tulikuwa
sahihi kwa kila mmoja wetu,” anakumbuka. “Wote tulikuwa hatujakamilika,
hakika tuliendana.”
Walioana kwenye harusi ya Kiislamu wakiwa na wageni 400 mnamo August 2008 na wamekuwa wenye furaha toka kipindi hicho.
Akaongeza: “Najiona nimebarikiwa sana kwa kukutana na Salima, ni mwanamke mzuri kwangu.
“Sasa naona kawaida
nina mke, ni kitu kikamilifu zaidi ya awali. Na sasa ana ujauzito wa
mtoto wetu wa kwanza nina furaha sana. Haijalishi kwa namna yoyote ile
nnavyoonekana ila sasa ni mwanaume mwenye furaha.”
Ila Latif, ambaye hana maumivu na hapati matibabu yoyote, anahofu mtoto wake kama anaweza kuzaliwa na hali kama aliyonayo yeye.
Anasema: “Hatuna uwezo
wa kumuona daktari, sisi ni masikini sana. Hakuna daktari kwa siku za
nyuma aliyenieleza nisipate mtoto. Ninakuwa na tumaini na kuomba kwamba
mtoto wetu atakuwa mwenye afya.”
Kaka yake na Latif
aliamua kuuza sehemu ya ardhi miaka minane iliyopita ili aweze kulipia
safari ya kwenda kumuona daktari ila hakukuwa na namna ambayo wangeweza
kuifanya.
Anakumbuka: “Daktari
aliniambia kwamba hali yangu ilitokana na mionzi ya jua wakati mama
alipokuwa na ujauzito wangu. Ila sijui kama nahitaji kumuamini.
“Na sasa kuna vitu vingi vinanijia kichwani mwangu kwamba kufanya upasuaji inaweza kuwa ni kitu cha hatari sana.
Nimepoteza tumaini lote la msaada. “Hivi ndivyo nitakavyokuwa daima.”
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment