MAAJABU! Ama kweli dunia ina mambo na ya Mungu mengi! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mbezi- Maua jijini Dar aliyefahamika kwa jina moja la Neema, amelea ujauzito wake kwa miezi tisa yenye matumaini lakini siku ya kujifungua akaambulia kiumbe cha ajabu kilichofanana na nyoka aina ya chatu..
Neema anayedaiwa kujifungua Chatu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, awali Neema alikuwa akisumbuliwa na pepo wachafu hali iliyomfanya akatishe masomo ya sekondari na kuanza kwenda kanisani kila wakati kwa ajili ya maombi.
MAUZAUZA KILA MARA
Chanzo kilisema kuwa, kipindi chote hicho, Neema alikuwa akianguka na kutaja majina ya watu wa mtaani anapoishi kwamba ni wachawi, wengine wanahusika kumchukua yeye usiku na kwenda naye makaburini ambako humlisha nyama na kumnywesha damu za watu.




“Neema alikuwa akisumbuliwa na mapepo tangu akiwa mdogo na alikuwa anasumbua kweli kweli. Alipokuwa akipandisha ‘madudu’ yake hayo hakuna aliyeweza kumshika labda wanaume kama watano. Pia kuna wakati alikuwa akitaka kujiua kwa kujichoma kisu,” kilisema chanzo hicho.
Mama mzazi wa Neema.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Naye mama mzazi wa Neema ambaye hakupenda kujitambulisha kwa jina, alipozungumza na mwandishi wa habari huku majirani wakifurika nyumbani kwake, alisimulia jinsi mwanaye huyo alivyokuwa akiteseka kipindi chote tangu alipokuwa mdogo mpaka ikafika hatua amepata ujauzito huo na hatimaye kujifungua kiumbe kinachofanana na chatu.




“Ni mambo mengi ambayo tumeyapitia lakini siwezi kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa sababu mpaka leo hii tuko wazima japo mitihani ni kipimo cha maisha na hata hili lililotokea karibuni ni mtihani pia, ila kikubwa ni kuomba sana.
“Baada ya kupata huu ujauzito kuna wakati tulikuwa hatulali, akianza kulia ni usiku kucha, anasema kuna kitu kinambana kifuani. Tulipokuwa tukienda hospitali kwa ajili ya uchunguzi, vipimo vilionesha mtoto tumboni hachezi.

“Mimi kama mzazi, hayo mambo yaliyokuwa yanamtokea mwanangu nilikuwa nayaona kama maajabu f’lani hivi japokuwa kipindi hicho alikuwa mzima na mimi mwenyewe nilikuwa nikimsubiri mjukuu wangu kwa hamu, kumbe tunakuja kupokea kitu cha ajabu namna ile,” alisema mama huyo.




SIKU YA KUUMWA UCHUNGU
Iliendelea kudaiwa kuwa, kipindi chote cha ujauzito, Neema alikuwa mtu wa maombi, lakini siku ya kuumwa uchungu alikimbizwa hospitali (haikutajwa jina) na kujifungua kiumbe cha ajabu. Ndipo familia ikaamua kukaa kikao na kuamua kukizika kiumbe hicho kama chatu.




Mama Neema anasema: “Mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu, kilikuwa kama chatu halafu kina magamba na meno mawili marefu lakini hakikuwa hai. Tulishtuka sana, tukaona ni mkosi katika familia lakini tuliamua kukizika kile kiumbe.“Sikuona sababu ya kuwaonesha majirani zangu kwa kuwa kilikuwa kinatisha. Ila naona ni bora niwape taarifa kuwa, mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu.”

ALICHOSEMA ALIYEJIFUNGUA
Naye Neema mwenyewe alipozungumza kuhusu tukio hilo la ajabu, alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.




“Labda niwaulize mama zangu ambao tayari walishazaa kama tumbo huwa linapanda juu mpaka kifuani badala ya kushuka? Na nilikuwa nakabwa sana kuanzia kifuani mpaka kwenye koo, usiku sikuwa nalala kutokana na maumivu niliyokuwa nikiyapata mpaka nilipojifungua hicho kiumbe.
“Usione watu tunatembea, hatujijui tuna nini kwenye miili yetu. Leo hii yamenikuta mimi, kesho mtu mwingine. (huku akiwaangalia majirani) mi nawaomba ndugu zangu tukazane kumwomba Mungu kwani mimi maombi yamenisaidia sana.”
Chanzo ni gazeti la Amani via Gpl

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top