Baadhi ya mashabiki wa staa wa Bongo Movies, Aunty Ezekiel wameonyesha kuchukizwa na nguo anzaovaa staa huyo ukizingatia kwasasa ni mjamzito.
Kwa mara kadhaa Aunty amekuwa akibandika picha mtandaoni akiwa amevaa nguo ambazo "followers" na mashabiki wamekuwa wakisema hazifai kuvaliwa na mwanamke mjamzito, kitu ambacho aunty mwenyewe na baadhi ya mashabiki wamekuwa mara zote wakisema ni sawa kitu ambacho mara zote husababisha mabshano na hadi kutoleana lugha chafu.
Mbali na wengi kusema nguo anazovaa zinambana sana tumbo kitu ambacho sio kizuri wa ustawi wa kiumbe kilichopo tumboni,wapo wailosema mavazi hayo hayana heshma kwani kwa hali yake ya sasa inabidi ajistili nasio kujiweka wazi wazi kama anavyofanya sasa.
Mimi sio mjuzi sana wa maswala ya nguzo za wamama wajawazito ndiomana nimezileata hapa baadhi ya picha hizo ili wenye uelewa wa maswala haya watujuze kam ni sawa au sio sawa...kwani kuna baadhi ya dada zetu wanapenda sana kuigaaaaaaa.
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment