Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rapa nchini Afrika Kusini Nkululeko Habedi ameuawa baada ya kugombana na mpenzi wake wa kike.
Mdogo wa mwanamuziki huyo alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa alimuona kaka yake anapoteza maisha kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Ndugu wa mwanamuziki huyo ambao walishuhudia tukio hilo wamesema kuwa waliamka mapema kuelekea kwa kaka yao na baada ya kufika karibu na nyumba yake walisikia kelele zikitoka ndani, muda mfupi walimuona rapa huyo akiwa anatokwa na damu nyingi kutokana na kugombana na mpenzi wake kwa muda wa masaa mawili.
Polisi nchini humo wamesema kuwa mpenzi wake huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hizi ni baadhi ya kutoka eneo la tukio:
Watu wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye eneo la tukio
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment