Mtu mmoja anayetuhumiwa kutaka kushambulia mji mkuu wa Marekani Washington DC, aliomba kituo cha televisheni kimoja kumtembelea mahabusu na alipohojiwa na mwandishi wa habari kama asingekamatwa alisema alisema angehakikisha risasi inaingia kichwani kwa Obama.
Mwandishi wa kituo cha televisheni (WXIX-TV) alidai kuwa mtuhumiwa huyo, Christopher Lee Cornell alipiga simu kutoka jela ya Kentucky ambako anashikiliwa na kukiri kwamba anaunga mkono kundi la ISIS na alikuwa amepanga kuua ili kuilazimisha serikali ya Marekani kujiondoa kwenye mgogoro huo.
Kituo hicho cha televisheni kilirusha sehemu ya mahojiano hayo Ijumaa usiku masaa kadhaa baada ya wakili wa mtuhumiwa huyo hoja zake kushindikana wakati akijaribu kumtetea mtuhumiwa huyo.
Vile vile mtuhumiwa huyo aliyekiri kuwa angevamia majengo mbalimbali pamoja na balozi za Israel alisema: Kama mimi mnaniona ni gaidi vile vile wanajeshi wa Marekani ni magaidi kwa kuingia nchini kwao, kuiba mali zao, kuua watu na kubaka wanawake.”
Cornell, mwenye miaka 20, bado anaishi na wazazi wake na anaunga mkono kundi la ISIS. Aliendelea kusema kundi hilo liko Ohio na kila Jimbo. Alionya ya kuwa ‘tumejipanga sana kuliko hata mnavyofikiri.”
Endapo mahakama itamkuta na kosa anaweza kwenda jela kwa miaka 20. Cornell alikamatwa nje ya duka la silaha karibu na nyumbani kwake Januari 14 baada ya FBI kupata taarifa kuwa kijana huyo alinunua mashine mbili M-15 na risasi 600. Hata hivyo baba wa mtoto huyo anasema kuwa mwanaye amedanganywa na anajaribu kutafuta wakili atakayeweza kumsaidia kijana wake kisheria.
Watu wengi watafiti wa mambo na mwenendo wa mwanadamu wamesema kijana huyo amerubuniwa kwa kiasi kikubwa, hivyo ufahamu wake wa kawaida umeondolea na kuwekewa vitu tofauti na akili yake ya kawaida ndio maana ana ujasiri huyo alionao.
Kijana wa kawaida mwenye miaka 20 ni lazima awe amepitia mambo fulani ndipo aweze kuwa na ujasiri huo lakini angekuwa amekulia maisha ya kawaida bila kurubuniwa kiakili asingeweza kufanya hivyo. Na utafiti unaonyesha ni vijana wengi na watoto wanatumiwa kutekeleza matukio kama hayo baada ya kufanyiwa mafunzo maalumu ya kisaikolojia ambayo huwafanya waamini wanachokiamini na kutekeleza matukio bila kujali utu wao
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment