Imebainika kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo unaotajwa kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya aamini kirahisi kuwa mwanaume wa maisha yake nihuyo anayemtongoza wakati huo.Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya manne yenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambayo niNAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.

Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambuakuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona wamefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.Kama nilivyosema neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni

NAKUPENDA. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini. Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo vinavyoonesha kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha. Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa

 ASANTE katika yale anayofanya. Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume. Niishie hapa kwa kuwashauri wanaume kuwa wakitaka kuwateka wanamke kimapenzi watumie kwa vitendo maneno haya manne

Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top