Hekaheka
ya leo inatokea Shinyanga inahusu mwanamke aliyepigwa na jiwe na
kujeruhiwa shingoni kwa kutuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume
wa mtu.
Mwanamke huyo amesema kuwa alitoka
kumsindikiza mgeni wake wakati anarudi akapata lift ya pikipiki lakini
ghafla alishangaa kupigwa jiwe na watu anaowafahamu ambao ni mtu na mke
wake.
Mwanamke huyo amesema baada ya kupigwa
walisimama ili kuwauliza kwa nini wampige jiwe lakini waliwakimbia,
wakaenda mpaka nyumbani kwa watu hao, lakini hakuweza kuongea nao kwa
kuwa walijifungia mlango ndani.
Mwanamke anayetuhumiwa kumpiga jiwe
amesema sio kweli kwamba alimpiga jiwe mwanamke huyo na wala hakuwepo
kwenye ugomvi huo kwa kuwa yeye alikuwa amelala hivyo hajui chochote.
Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo
wanasema ni kweli waliomuona mwanaume na mke wake waliorusha mawe na
baada ya kurusha mawe hayo walikimbia kwenda kujifungia ndani ya nyumba
yao.
Bonyeza Hapa Chini kusikiliza Hekaheka yote hapa
Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog
Post a Comment