Majina ya Abiria Wote Waliokuwa Katika Ajali iliyouwa Watu Iiringa Jana

"Ni ajali ambayo haijawahi kutokea katika maeneo haya," ni baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wakazi wengi wa mjini Mafinga na vitongoji vyake, ambao jana walishuhudia ajali  katika historia ya mji huo.
Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26)  na basi aina ya Scania namba T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).

Wakati lori lilikuwa likielekea Barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 42 wakiwemo 40 waliokuwemo katika basi na wawili katika lori hilo, ilitokea katika eneo la Changarawe takribani kilometa 5 kutoka mjini Mafinga, mkoani Iringa, katika barabara kuu ya Mafinga-Mbeya.

Kati ya waliokufa yupo dereva wa basi hilo, huku dereva wa lori akijeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa na kitu kama nondo shingoni mwake.
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi saa tatu na nusu.

Kamanda Mungi alisema jeshi lake kwa kushirikiana na hospitali za Mafinga na Mkoa wa Iringa wanaendelea kutambua majina ya watu waliokufa na  majeruhi.

Kamanda Mungi alisema taarifa zao za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara. Mungi alisema lori na basi hilo yaligongana uso kwa uso wakati madereva wake wakishindana kuwahi kuchepuka moja kati ya mashimo makubwa yaliyopo pembezoni na katikati mwa barabara hiyo katika eneo hilo.

Baadhi ya watu waliotajwa kuwepo katika basi na lori hilo ambao hata hivyo hawakuweza kufahamika mara moja, nani kafa na nani kajeruhiwa ni pamoja na Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni na Frank Chiwango.

Wengine ni Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine, Mwajengo, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri.

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge na Juma Sindu.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Habari kutoka Mbeya zinaeleza kuwa wakati basi hilo linaondoka kituoni abiria waliokuwepo kwenye basi hilo walikuwa ni 37 ambao ni: 

Baraka Ndone  ambaye ni dereva, Yahya  Hassan ambaye ni kondakta, Esther    Emmanuel, Henry Lugano, Lusekelo Enock, Jeremia  Watson, Hamad, Olga Solomon, Neto, Theresia Kaminyoge, Frank Chiwanga, Luteni Sanga, Alfred Sanga, Doto Katunga,  Juliana Bukuku, Esther Fidel,  Paulina Josia.

Wengine ni Iman Mahenge,  Catherine Mwate, Mathias Justine,  Rebeka Kasambala,  Upendo William, Mbamba Ipyana,  Ndulile Kasambala, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule, Mustafa Ramadhani,  Musa, Omega Mwakasege, Shadra Msigwa, Lucy Mtanga, Charles Mweisonga, Martin Haule, Dominick Mashauri, Kelvin Ebadi, Juma Saidi,  na Nicko.


Shiriki nasi kwa kutoa maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Michapo Blog

Post a Comment

 
Top